Tamasha la Teknolojia la Afrika lafunguliwa kwa kuangazia fursa za AI

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2026

Watu wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Teknolojia la Afrika 2026 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 17, 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

Watu wakihudhuria hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Teknolojia la Afrika 2026 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 17, 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

CAPE TOWN - Tamasha la Teknolojia la Afrika 2026 limefunguliwa rasmi Jumanne wiki hii mjini Cape Town, Afrika Kusini, kwa kujikita katika kuendeleza mabadiliko ya kidijitali kote barani humo na kuiwezesha Afrika kutumia fursa katika zama ya akili bandia (AI).

Tamasha hilo, ambalo linafanyika kwa mara ya 29 mwaka huu ni moja ya shughuli kubwa na zenye ushawishi zaidi za teknolojia barani Afrika, likiwaleta pamoja viongozi wa sekta za mawasiliano na teknolojia, wajasiriamali, wawekezaji, watunga sera na wavumbuzi, na linafanyika chini ya kaulimbiu kuu "Kusukuma mbele mabadiliko ya kidijitali ya Afrika".

Shughuli hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia maeneo sita makuu ya maudhui yaliyounganishwa, ambazo ni Mawasiliano ya Simu na Muunganisho, Vituo vya Data, AI, Usalama wa Mtandao, Kampuni Changa na Mabadiliko Makubwa ya Kidijitali, yanayohusisha maeneo muhimu kuanzia miundombinu ya kidijitali na teknolojia zinazoibuka hadi ujasiriamali na ukuaji wa uchumi wa kidijitali wa Afrika.

Naibu Rais wa Afrika Kusini, Paul Mashatile, akitoa hotuba kwa njia ya mtandao kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Teknolojia la Afrika jijini Cape Town, Afrika Kusini, tarehe 17 Novemba 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

Katika hotuba ya ufunguzi mtandaoni, Naibu Rais wa Afrika Kusini Paul Mashatile ametoa wito kwa nchi za Afrika kushiriki kikamilifu zaidi katika kuunda mwelekeo wa mazingira ya AI duniani, akisema Afrika lazima iwe mwendelezaji na muuzaji nje wa teknolojia zinazoibuka badala ya kubaki kuwa mtumiaji wa suluhisho zilizotengenezwa kwingineko.

"Lazima tuwe washiriki hai katika kuendeleza, kutumia na kusimamia teknolojia hizi, kuhakikisha zinasaidia kutimiza malengo yetu ya maendeleo na kuchangia katika mustakabali jumuishi na wenye ustawi zaidi," alisema.

Watu wakizungumza kwenye eneo la maonesho katika Tamasha la Teknolojia la Afrika 2026 jijini Cape Town, Afrika Kusini, tarehe 17 Novemba 2026. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha