Mkutano wa Watendaji Wakuu wa APEC 2026 watoa Pendekezo la Shenzhen linalotoa wito wa ustawi wa pamoja katika Asia-Pasifiki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 19, 2026

SHENZHEN - Pendekezo la Shenzhen la Mkutano wa Watendaji Wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia-Pasifiki (APEC) 2026 limetolewa jana Jumatano, likitoa wito wa kuendeleza kwa kina uchumi wa kikanda ulio wa kufunguliwa mlango, kuchochea ongezeko la uchumi la shirikishi kupitia uvumbuzi wa teknolojia, kuimarisha mafungamano ya mawasiliano ya habari ya kikanda, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kufikia ustawi wa pamoja.

Hii ni mara ya kwanza kwa nyaraka za mafanikio ya mkutano kutolewa kama pendekezo katika historia ya miaka 30 ya mkutano huo.

Pendekezo hilo linaeleza kuwa, chini ya miongozo ya maeneo manne muhimu, yanayohusu ufunguaji mlango na shirikishi, ukuaji unaoendeshwa na uvumbuzi, mafungamano ya mawasiliano ya habari ya karibu zaidi na ushirikiano wa kunufaishana, wafanyabiashara wa Asia-Pasifiki wako tayari kufanya ushirikiano na makundi yote ya uchumi ili kutekeleza kivitendo kwa pande zote Matarajio ya Putrajaya 2040 na kujenga jumuiya ya Asia-Pasifiki iliyo ya kufunguliwa mlango, inayojaa nguvu hai, na yenye himilivu na ya amani.

Pendekezo hilo pia limetoa wito wa kubadilisha kaulimbiu ya APEC ya mwaka huu ya "Kujenga Jumuiya ya Asia-Pasifiki yenye Mustakabali wa Pamoja, Kustawi Pamoja," kuwa vitendo halisi, ili eneo la Asia-Pasifiki liendelee kuwa injini ya ongezeko la uchumi yenye nguvu hai zaidi duniani, na jumuiya yenye ustawi wa pamoja. 

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha