Lugha Nyingine
Ni kwa namna gani tunda la duriani linasafirishwa kuvuka eneo la Asia-Pasifiki hadi mezani?
Kwenye bustani ya Malaysia, picha iliyopigwa kwa simu inaruhusu AI kusaidia wakulima kuhesabu matunda ya duriani kwenye picha. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shenzhen Bao'an, mjini Shenzhen, China, roboti za kukagua matunda huhakiki kiotomatiki lebo, vielelezo na taarifa zingine, hali inayofanya uidhinishaji wa forodha kuwa wenye ufanisi zaidi.
Mara tu yanapokuwa yamekaguliwa na kuidhinishwa na forodha, matunda freshi ya duriani yanaweza kufikia meza za walaji wa China ndani ya muda mfupi kama saa mbili tu. Kutoka kwenye tawi la mti hadi mezani, safari ya tunda la duriani ya kuvuka bahari huleta pamoja teknolojia, uchukuzi na biashara—ikigeuza manufaa ya ufunguaji mlango na ushirikiano kote katika eneo la Asia-Pasifiki kuwa ladha tamu ya maisha ya kila siku.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma