Lugha Nyingine
Zambia yaweka jiwe la msingi la kiwanda chake cha kwanza cha kuzalisha chanjo pamoja na China
Zambia imeweka jiwe la msingi la kiwanda chake cha kwanza cha kuzalisha chanjo Jumanne wiki hii mjini Lusaka, ikiwa ni hatua kuelekea uzalishaji wa ndani wa chanjo na kuimarisha usalama wa afya.
Kiwanda hicho kitajengwa na ZAMVAX, kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo ya Vidwanda (IDC) na Kampuni ya Jijia ya Teknolojia ya Matibabu ya China, ukiwa na mgawanyo wa hisa wa aslimia 60 kwa 40, katika Eneo la Kiuchumi la Kusini mwa Lusaka.
Katika kipindi cha kwanza cha ujenzi wa mradi huo, kituo cha kujaza na kukamilisha uzalishaji wa chanjo ya kipindupindu ya kumeza, kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha takriban dozi milioni 20 kwa mwaka. Kipindi kitakachofuata kinatarajiwa kuanzisha uzalishaji wa antijeni za kienyeji, zitakazowezesha uzalishaji kamili wa chanjo ya kipindupindu kutoka mwanzo hadi mwisho. Licha ya hayo, mradi huo pia unatarajiwa kupanuka na kuingia katika uzalishaji wa chanjo za watoto na wanyama.
Sherehe ilihudhuriwa na mshauri wa Balozi wa China nchini Zambia Wang Sheng, Waziri wa Afya wa Zambia Roma Chilengi, na maafisa wengine wakuu wa serikali na wawakilishi wa kampuni ya China.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma