Lugha Nyingine
Mfumo wa miamala ya RMB ya kuvuka mipaka wazinduliwa Botswana
Benki ya Stanbic Botswana jana Jumanne mjini Gabaorone ilizindua ufikiaji wa moja kwa moja wa Mfumo wa Malipo ya kuvuka Mipaka (CIPS), ikiwa benki ya kwanza nchini humo kutoa huduma hiyo.
CIPS ni mfumo wa miundombinu ya kifedha wa China unaowezesha malipo ya kuvuka mipaka na utatuzi wa sarafu ya China, renminbi (RMB), na kuzipa taasisi wanachama za kifedha njia maalum ya miamala ya kimataifa.
Balozi wa China nchini Botswana Fan Yong alisema huduma hiyo inaweza kufupisha muda wa kufanya malipo, kupunguza hatari za miamala na kufanya malipo ya RMB kuwa rahisi zaidi. Amesema kuinuliwa kwa mahusiano ya pande mbili hadi ushirikiano mpana wa kimkakati kati ya China na Botswana, kutatoa matokeo ya kivitendo kwenye biashara, uwekezaji, uchimbaji madini, kilimo, teknolojia na huduma za afya.
Bw. Fan amesema thamani ya biashara kati ya China na Botswana ilifikia dola za Marekani bilioni 1.222 mwaka wa 2025, na katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, iliongezeka kwa asilimia 58.6 hadi kufikia dola milioni 852 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Maonesho ya picha ya China na Afrika yazidisha urafiki na uhusiano wa kiutamaduni

Maua mabichi yaliyokatwa ya Kenya yang’ara kwenye soko la China

Maonyesho ya urukaji wa ndege yafanyika Changchun kuadhimisha kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la China

Shughuli ya Siku ya Meli ya "Xuelong 2" ya China kufunguliwa kwa umma yafanyika Hainan
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma