Mfuate Xi | Kwenda kwenye Shenzhen pamoja na Asia-Pasifiki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2026

Katika Mji wa Shenzhen, China, tunda la duriani kutoka Malaysia linaweza kufika kwenye meza ya walaji ndani ya muda mfupi kama saa mbili tu baada ya kukaguliwa na kuidhinishwa kwenye forodha katika uwanja wa ndege. Usafirishaji mzigo kwa kutumia droni na roboti kwenye biashara ya rejareja vinazidi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya mjini. Katika eneo la Asia-Pasifiki, Reli ya Mwendo-Kasi ya Jakarta–Bandung inaleta manufaa ya ushirikiano kati ya China na Indonesia kwa umma wa kawaida; wakati huohuo kiwanda cha BYD nchini Thailand, wafanyakazi Wachina na Wathailand wanafanya kazi bega kwa bega kuzishinda changamoto za kiteknolojia na kuchangia katika fursa za maendeleo ya kiwanda.

"Ufunguaji mlango ni pumzi ya maisha ya ushirikiano wa Asia-Pasifiki”“Uvumbuzi ni nguvu muhimu inayoongoza maendeleo ya dunia”“Ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote ni njia sahihi katika dunia ambayo inazidi kuwa pana zaidi”... China chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping inafungua mlango kwa ngazi ya juu zaidi ili kuiunganisha Asia-Pasifiki na kuunda fursa kupitia ushirikiano wa kivumbuzi.

Mkutano wa 33 wa Kawaida wa Viongozi wa APEC utafanyika Shenzhen kuanzia tarehe 18 hadi 19, Novemba. Kwa mwelekeo wa ufunguaji mlango, uvumbuzi na ushirikiano, Shenzhen iko tayari kukaribisha wageni kutoka sehemu mbalimbali za Asia-Pasifiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha