Lugha Nyingine
Wabunge wa kimataifa wakusanyika Nairobi kujadili namna ya kukabiliana na njaa
(CRI Online) Novemba 17, 2026
Zaidi ya wabunge 250 na wajumbe kutoka sehemu mbalimbali duniani wamekutana Nairobi Novemba 16 kwenye mkutano unaojadili njaa, utapiamlo na mifumo endelevu ya kilimo cha chakula.
Rais William Ruto wa Kenya alifungua Mkutano wa tatu wa Bunge la Kimataifa Dhidi ya Njaa na Utapiamlo, na kuwataka wabunge kutumia mageuzi ya kisheria, usimamizi, na ufadhili katikakuimarisha usalama wa chakula na lishe duniani.
Rais Ruto amesema "Kukomesha njaa kunahitaji sheria, bajeti na usimamizi, na haya ni majukumu ya msingi ya mabunge."
Mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, na umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Bunge la Kenya na Shirika la Hispaniala Ushirikiano wa Kimataifa wa Maendeleo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



