Lugha Nyingine
Mabalozi na mjumbe maalum wa China wafanya ziara katika nchi saba za Mashariki ya Kati, Ghuba na Afrika ili kupunguza mivutano
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema, hivi karibuni mabalozi maalum na mjumbe maalum wa China wameanza kufanya ziara katika nchi saba za Mashariki ya Kati, Kanda ya Ghuba na Pembe ya Afrika. Ziara hizo ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za China katika kupunguza mivutano na kukomesha uhasama.
Bi. Mao amesema, mabalozi na mjumbe hao ni pamoja na mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Mashariki ya Kati Balozi Zhai Jun, mjumbe maalum wa mambo ya Afrika wa serikali ya China Balozi Liu Xianfa, na mjumbe maalum anayeshughulikia mambo ya Pembe ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Balozi Hu Changchun.
Katika ziara hizo mabalozi maalum na mjumbe maalum wamekutana na viongozi wa nchi husika, mawaziri wa mambo ya nje na maofisa wengine wanaoshughulikia mambo ya nje na usalama wa taifa. Bi. Mao ameongeza kuwa wamefanya mazungumzo kuhusu kuimarisha uhusiano wa pande mbili, huku wakibadilishana maoni kwa kina na pande zote kuhusu kuhimiza kupunguza mivutano ya kikanda na kufikia maelewano kadhaa ya pamoja juu ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kulinda amani na kukuza maendeleo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



