Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China awasili Manila kuhudhuria mkutano wa viongozi wa China na ASEAN
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2026

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili Manila, Ufilipino, Novemba 15, 2026. (Xinhua/Ding Haitao)
MANILA - Waziri Mkuu wa China Li Qiang amewasili Manila jana Jumapili kwa kuhudhuria kwenye Mkutano wa 29 wa Wakuu wa China na Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) kutokana na mwaliko wa Rais Ferdinand Romualdez Marcos Jr wa Ufilipino, ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa ASEAN.
Li amewasili katika mji mkuu huo wa Ufilipino baada ya kumaliza ziara yake rasmi nchini Thailand na atahudhuria kwenye Mkutano wa viongozi wa China na ASEAN leo Jumatatu.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili Manila, Ufilipino, Novemba 15, 2026. (Xinhua/Huang Jingwen)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



