Lugha Nyingine
WHO yaonya kuwa mlipuko wa Ebola nchini DRC bado unaleta hali ya wasiwasi
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa, mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado unaleta hali ya wasiwasi huku mamia ya magonjwa walioambukizwa wakiripotiwa kila wiki, na kuongezeka kwa vurugu kunatishia kudhoofisha maendeleo yaliyopatikana katika miezi kadhaa ya kudhibiti ugonjwa huo.
Mkurugenzi wa WHO anayeshughulikia masuala ya dharura kanda ya Afrika, Marie Roseline Belizaire ameonya kuwa, maambukizi yanaendelea kuenea katika maeneo mapya licha ya kupungua katika baadhi ya maeneo ya mwanzo ya mlipuko. Amesema, karibu miezi sita baada ya mlipuko kutangazwa, DRC bado inaripoti kesi karibu 400 hadi 500 kila wiki.
Kwa mujibu wa ripoti ya hali ya hivi karibuni iliyotolewa na mamlaka za afya za DRC, mpaka kufikia jumanne wiki hii, nchi hiyo imerekodi kesi 11,114 zilizothibitishwa, ikiwemo vifo 5,433, huku kiwango cha vifo kikifikia asilimia 48.9.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



