Tanzania kupanua matumizi ya nishati mbadala ili kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme

(CRI Online) Novemba 13, 2026

Tanzania inapanga kuzalisha megawati 1,892 za umeme kutoka vyanzo vya nishati mbadala ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza uwezo wa jumla wa nchi wa kuzalisha umeme kufikia megawati 8,000.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Nishati anayesimamia sekta ya mafuta na gesi, James Mataragio, amesema hayo wakati akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Wiki ya Nishati Mbadala ya mwaka 2026 jijini Dar es Salaam. Mataragio amesema, vyanzo vya nishati mbadala, ikiwemo nishati ya jua, upepo na nishati itokanayo na viumbe hai, vitakuwa na mchango mkubwa katika kufikia lengo la kitaifa la uzalishaji wa umeme.

Amesema, Dira ya Maendeleo ya nchi hiyo ya mwaka 2050 inalenga kufikia uwezo wa kuzalisha umeme wa gigawati 70 ifikapo mwaka 2050.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha