Rais Xi Jinping wa China kuhudhuria Mkutano wa 33 usio rasmi wa viongozi wa APEC

(CRI Online) Novemba 13, 2026

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, amesema mkutano wa 33 usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC) utafanyika Novemba 18 na 19 mjini Shenzhen, ukiwa na kaulimbiu ya “Kujenga Jumuiya ya Asia na Pasifiki, Kuhimiza Ustawi wa Pamoja.”Rais Xi Jinping wa China ataongoza mkutano huo na kutoa hotuba.

Wakati mkutano huo utakapofanyika, Rais Xi pia ataandaa dhifa ya kuwakaribisha viongozi na wajumbe wa nchi mbalimbali watakaohudhuria mkutano na kufanya mkutano wa pande mbili na viongozi wa nchi za nje.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha