Mgonjwa wa mwisho wa Ebola nchini Kenya aruhusiwa kuondoka hospitali

(CRI Online) Novemba 12, 2026

Wizara ya Afya ya Kenya imesema, mgonjwa wa mwisho wa Ebola nchini humo amepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini, na watu 11 wa mwisho waliokuwa na mawasiliano ya karibu na wagonjwa waliothibitishwa wamekamilisha kipindi chao cha ufuatiliaji cha siku 21 na kuondolewa kwenye karantini.

Akizungumza hapo jana, Waziri wa Afya wa Kenya Aden Duale amesema, kulikuwa na jumla ya visa 9 vilivyothibitishwa katika mlipuko wa sasa wa Ebola nchini humo, ikiwemo vifo 2. Jumla ya watu 135 waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa walifuatiliwa, na visa vyote vilidhibitiwa ndani ya mnyororo mmoja wa maambukizi, bila kuwepo kwa maambukizi yoyote katika jamii.

Duale amesema, kuanzia leo, Kenya itaanza kipindi cha ufuatiliaji cha siku 42, na kama hakuna visa vipya vitakavyoripotiwa katika kipindi hiki, mlipuko wa Ebola nchini humo unatarajiwa kutangazwa rasmi kumalizika Desemba 23.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha