Viongozi duniani wakusanyika katika mkutano wa COP31, wakitoa wito wa hatua za haraka za tabianchi, mageuzi ya mfumo wa ufadhili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2026

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026 ikionesha mlango wa kuingilia kwenye ukumbi wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Antalya, Uturuki. (Xinhua/Liu Lei)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026 ikionesha mlango wa kuingilia kwenye ukumbi wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Antalya, Uturuki. (Xinhua/Liu Lei)

ANTALYA, Uturuki - Mkutano wa Viongozi wa Antalya wa Mkutano wa 31 wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP31) umefunguliwa rasmi jana Jumatano, kwa kujikita katika kubadilisha ahadi za tabianchi kuwa hatua halisi.

Akifungua mkutano huo wa ngazi ya juu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehimiza ushirikiano wa kimataifa katika changamoto za pamoja. "Hatuhitaji nchi kukubaliana kila kitu, lakini tunazihitaji zishirikiane katika mambo ambayo hakuna nchi inaweza kuyatatua peke yake," amesema.

Akizungumzia mabadiliko katika sekta ya nishati, Guterres ameongeza kuwa nishati ya jua pekee ilikidhi karibu robo tatu ya ukuaji wa mahitaji ya umeme duniani mwaka jana, ikithibitisha kwamba nishati safi imekuwa chanzo cha bei nafuu zaidi cha uzalishaji wa umeme mpya katika sehemu nyingi duniani.

Mkutano huo wa mwaka huu unalenga kuziba pengo kati ya malengo makubwa na utimizaji wa utekelezaji, utoaji wa fedha, na uhimilivu wa tabianchi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema, "Mataifa yaliyoendelea, ambayo kihistoria yamekuwa yakitumia bajeti ya kaboni duniani, lazima yachukue wajibu mkubwa zaidi katika kupunguza uzalishaji wa hewa chafu na kutoa ufadhili."

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese amesisitiza kwamba ushirikiano wa kimataifa unawezesha uwekezaji kwenye nishati safi na kuharakisha ufadhili wa tabianchi, huku akisisitiza kwamba "hakuna yeyote anayepaswa kuachwa nyuma" katika mpito wa nishati safi.

Picha hii, iliyopigwa Novemba 11, 2026 ikionesha banda la Uturuki kwenye eneo la kufanyika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Antalya, Uturuki. (Xinhua/Liu Lei)

Picha hii, iliyopigwa Novemba 11, 2026 ikionesha banda la Uturuki kwenye eneo la kufanyika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Antalya, Uturuki. (Xinhua/Liu Lei)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026 ikionesha ukumbi wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Antalya, Uturuki. (Xinhua/Liu Lei)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026 ikionesha ukumbi wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa, Antalya, Uturuki. (Xinhua/Liu Lei)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha