Russia na Ukraine zamaliza mazungumzo kwenye Abu Dhabi kwa kubadilishana wafungwa huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2026

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

ABU DHABI - Mazungumzo ya pande tatu yanayohusisha Russia, Marekani na Ukraine yamemalizika jana Jumatano jijini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo Russia na Ukraine zimefikia makubaliano ya kubadilishana wafungwa kwa "idadi kubwa."

Vladimir Medinsky, mkuu wa ujumbe wa Russia kwenye mazungumzo kuhusu mgogoro wa Ukraine, ameuambia mkutano na waandishi wa habari kuwa maelezo ya ubadilishanaji huo wafungwa yatatangazwa hivi karibuni na kwamba mazungumzo yataendelea.

Amesema wajumbe walijadili masuala ya kibinadamu, huku mustakabali wa usalama wa Ulaya ukiwa ni jambo kuu katika mazungumzo hayo yaliyopatanishwa na Marekani.

Medinsky ameongeza kuwa pande husika zimefikia maelewano juu ya baadhi ya masuala, bila kutoa maelezo zaidi.

Ametetea hitaji la kujadili mipango ya usalama wa baada ya vita katika hatua ya sasa ya mazungumzo, akisema kuwa mgogoro nchini Ukraine umefichua mapungufu katika mfumo wa usalama wa Ulaya.

Medinsky ametoa wito wa kuundwa kwa mfumokazi wa usalama ulio wa haki ambao unazingatia maslahi ya nchi zote.

Kuhusu ushiriki wa Ulaya, Medinsky amesema ujumbe wa Russia haukufanya mazungumzo na wawakilishi wa Ulaya jijini Abu Dhabi na hauelewi nafasi yao kwenye mazungumzo hayo.

Medinsky amekosoa uongozi wa baadhi ya nchi za Ulaya kwa kufadhili na kutoa silaha kwa Ukraine, akiwashutumu kwa kuchangia vifo vya raia na kurefusha muda wa mgogoro huo.

Amesema Moscow haijapokea mipango au mapendekezo yoyote ya amani kutoka kwa nchi za Ulaya, na hivyo haioni sababu ya kufanya mazungumzo nazo kwa sasa. Hata hivyo, amedokeza kuwa Russia iko tayari kuzingatia mapendekezo madhubuti kama yatawasilishwa.

Wakati huo huo, Jared Kushner, mjumbe wa timu ya mazungumzo ya Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo hayo yalikuwa ya kina na yaligusia masuala yote makuu.

Pia amesema yeye na mjumbe maalum wa Marekani, Steve Witkoff, wanapanga kusafiri hadi Moscow kwa ajili ya majadiliano zaidi kuhusu kumaliza mgogoro huo wa Ukraine.

Kwa upande wa Ukraine, mpatanishi David Arakhamia, ambaye ni mwenyekiti wa kundi la wabunge wa chama cha kisiasa cha Ukraine kiitwacho 'Servant of the People', amesema mazungumzo hayo ya Abu Dhabi yameleta "msukumo mzuri" kuelekea kupata suluhisho la mgogoro huo kabla ya mwisho wa mwaka.

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

Picha hii iliyopigwa Novemba 11, 2026, ikionesha mandhari ya jiji la Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu. (Xinhua/Wang Zecong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha