China na Namibia zaadhimisha miaka 30 ya ushirikiano wa timu za madaktari

(CRI Online) Novemba 12, 2026

China na Namibia zimeadhimisha miaka 30 tangu timu ya kwanza ya madaktari wa China kuwasili Namibia, huku maofisa wakielezea mafunzo ya afya, afya ya kidijitali na upatikanaji mpana wa huduma za kitaalamu kama vipaumbele vya ushirikiano wa baadaye.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Windhoek, mji mkuu wa Namibia, Naibu Waziri wa Afya na Huduma za Jamii wa nchi hiyo Suzan Ndjaleka amesema, miongo mitatu ya ushirikiano imezipa nchi hizo mbili msingi imara wa kufanya kazi kwa karibu zaidi. Ameongeza kuwa, awamu ijayo ya ushirikiano huo inapaswa kuwa na uratibu wa kina zaidi wa kitaasisi na kupanua maendeleo ya fursa za kitaaluma, utafiti, uvumbuzi, na ujenzi endelevu wa uwezo.

Naye Naibu Mkurugenzi wa Tume ya Afya kutoka mkoa wa Zhejiang nchini China, Yu Xinle, ameahidi kuendeleza ushirikiano wa afya chini ya hatua za uhusiano wa China na Afrika, zikilenga kuanzisha kwa pamoja hospitali maalum, mafunzo kwa wataalamu wa afya na ujenzi wa uwezo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha