Wang Yi afanya mazungumzo ya kuhimiza hamasa na ya kiujenzi na Rubio juu ya uhusiano kati ya China na Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2026

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amefanya mazungumzo ya kuhimiza hamasa na ya kiujenzi kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio.

Kwenye mazungumzo hayo yaliyofanyika jana Jumatano pande hizo mbili zimebadilishana maoni kwa kina juu ya uhusiano kati ya China na Marekani na mazungumzo kati ya marais wa nchi hizo mbili.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuwa ziara ya Rais Xi Jinping nchini Marekani mwezi Septemba ilikuwa imefanyika vizuri na kupata mafanikio.

Amesema wakuu hao wawili wa nchi mbili walikubaliana kuongeza matarajio mapya ya uhusiano kati ya China na Marekani, wakitoa mwongozo wa kimkakati ulio wazi zaidi kwa ajili ya kutafuta njia ya kutendeana kati ya nchi hizo mbili.

"Mwelekeo huu tulivu wa uhusiano kati ya China na Marekani haujapatikana kwa urahisi na ni chaguo la busara la nchi kubwa hizi mbili kutokana na maslahi yenyewe ya kila nchi kati yao pamoja na maslahi yao ya pamoja." Wang amesema.

Wang amesema, siku zote China inadumisha sera tulivu na isiyobadilika kuhusu Marekani, inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na upande wa Marekani, kushughulikia ipasavyo migongano na masuala nyeti, kuungana mkono katika kuandaa Mkutano wa Viongozi wa Uchumi wa APEC 2026 na Mkutano wa Viongozi wa G20, na kufanya juhudi za kuhimiza uhusiano wa kiujenzi wenye utulivu wa kimkakati kati ya China na Marekani upate matokeo halisi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha