Lugha Nyingine
China yataka jumuiya ya kimataifa kusaidia Sudan Kusini kufanya uchaguzi kwa utaratibu
Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Sudan Kusini kufanya uchaguzi kwa utaratibu kwa kutoa msaada wa vifaa na teknolojia kwa ajili ya uchaguzi huo.
Balozi Sun amesema hayo alipohutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Sudan Kusini. Amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kusaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto ikiwemo ukosefu wa rasilimali za uchaguzi, na kuunga mkono utekelezaji wa kazi wa taasisi za uchaguzi, ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utaratibu.
Balozi Sun pia amesisitiza kuwa China inaunga mkono Sudan Kusini kulinda haki, uhuru na ukamilifu wa ardhi yake, pia inaunga mkono wananchi wa Sudan Kusini kutafuta njia ya kujiendeleza inayolingana na hali ya nchi yake.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



