Wahamiaji 171 wa Somalia warudi nyumbani kutoka Libya

(CRI Online) Novemba 11, 2026

Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) limetangaza kuwa wahamiaji 171 wa Somalia wamerudi nyumbani kutoka Libya chini ya mpango wa kurudi kwa hiari wa kibinadamu unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya.

Shirika hilo limetoa taarifa kwenye mtandao wa kijamii ikisema, wahamiaji wamerudi kutoka miji ya Benghazi na Sabha ya Libya hadi Hargeisa na Mogadishu nchini Somalia.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa msaada wa kibinadamu umetolewa kutokana na mahitaji ya kila mhamiaji. IOM imesisitiza tena ahadi yake ya kuwasaidia wahamiaji wanaotaka kurudi nyumbani kwa hiari, usalama na heshima.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha