Marekani yasema hakuna haja ya kufanya operesheni kubwa za kijeshi dhidi ya Iran

(CRI Online) Novemba 11, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, amesema, vikwazo vya kiuchumi na vizuizi vya baharini vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran vimepata mafanikio makubwa, hivyo hakuna haja ya kufanya operesheni kubwa za kijeshi dhidi ya nchi hiyo.

Rubio amesema hayo jana baada ya kushiriki kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi saba uliofanyika Paris, Ufaransa. Amesema Marekani bado inashikilia msimamo wa wazi kwa kufikiwa kwa "makubaliano halisi," lakini masharti yaliyotolewa na Iran hayana msingi wowote, na kuongeza kuwa, rais wa Marekani Donald Trump amekataa waziwazi madai ya Iran kuhusu fidia ya uharibifu wa mali kutokana na vita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha