Jukwaa la Ushirikiano wa Washauri Bingwa la BRI na Jukwaa la Utangazaji wa Kimataifa yaanza Xi'an, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 11, 2026

Washiriki wakionekana kwenye Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 la Utangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Novemba 10, 2026. (Xinhua/Li Yibo)

XI'AN - Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 laUtangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) yamefunguliwa huko Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, jana Jumanne.

Majukwaa hayo yana kaulimbiu ya "Kufanya Ushirikiano wa Sifa Bora ya Juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, Kuhimiza Kufundishana kati ya Ustaarabu na Kufanya Ujenzi wa Mambo ya Kisasa," na yanalenga kukusanya hekima za dunia nzima na kuhimiza maendeleo mapya ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja wa sifa bora kwenye kiwango cha juu zaidi.

Wanadiplomasia, wataalamu wa jumuiya za washauri bingwa, waandishi wa habari, wataalamu wa utamaduni na utalii na wajumbe wa biashara zaidi ya 300, kutoka nchi na maeneo zaidi ya 50 wanahudhuria kwenye mkutano wa majukwaa hayo wakishiriki katika kubadilishana mawazo na kufanya majadiliano.

Katika hotuba yake, Zhao Gang, naibu katibu wa Kamati ya Chama cha CPC ya Mkoa wa Shaanxi na ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, amesema kwamba katika miaka ya hivi karibuni mkoa huo umejifungamanisha kwa kina katika muundo mpana zaidi wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Lyu Yansong, mhariri mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua, amesema kwamba katika miaka 13 iliyopita, ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja umekua kutoka matarajio hadi kuwa miradi halisi na dhahiri ya ushirikiano, ikitoa mchango wa kuhimiza hamasa kwa ajili ya kuongeza urafiki kati ya China na nchi washirika na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi washirika.

Amesema akiwa kiongozi wa Baraza la Waanzilishi wa Mtandao wa Utafiti wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRSN), shirika la Xinhua liko tayari kufanya juhudi pamoja na wenzake wa ndani na nje ya China ili kuzidisha utafiti na uelezeaji wa maana ya ushirikiano wa sifa bora ya juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuonesha mafanikio yenye matunda mengi ya nchi washirika katika kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa na kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali, na pia kukusanya nguvu kubwa kwa ushirikiano wa sifa bora ya juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

BRSN imeendelea kupanua ushawishi wake tangu kuanzishwa kwake miaka saba iliyopita. Kwenye hafla ya ufunguzi, taasisi nne mpya ambazo ni Jukwaa la Kimataifa la BRICS, Chuo Kikuu cha Xi'an Jiaotong, Chuo cha Kitaifa cha Manas cha Jamhuri ya Kyrgyzstan, na Kituo cha Mkakati wa Maendeleo cha Uzbekistan zilikabidhiwa nyaraka kwa ajili ya kusaini.

Ripoti ya jumuiya ya washauri bingwa yenye kichwa cha "Kujenga Uchumi wa Uwazi wa Dunia Kupitia Ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja" ilitolewa duniani kote kwa Kichina na Kiingereza.

Majukwaa hayo yanaandaliwa kwa pamoja na Shirika la Habari la China, Xinhua, Kamati ya Chama na Serikali za Mkoa wa Shaanxi.

Picha iliyopigwa Novemba 10, 2026 ikionesha mwonekano wa Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 la Utangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China. (Xinhua/Li Yibo)

Picha iliyopigwa Novemba 10, 2026 ikionesha mwonekano wa Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 la Utangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China. (Xinhua/Li Yibo)

Washiriki wakionekana kwenye Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 la Utangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Novemba 10, 2026. (Xinhua/Li Yibo)

Washiriki wakionekana kwenye Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 la Utangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, Novemba 10, 2026. (Xinhua/Li Yibo)

Picha iliyopigwa Novemba 10, 2026 ikionesha mwonekano wa Jukwaa la Ukanda Mmoja, Njia Moja la Ushirikiano wa Kimataifa wa Jumuiya za Washauri Bingwa 2026 na Jukwaa la 4 la Utangazaji wa Kimataifa la Njia ya Hariri (Xi'an) huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China. (Xinhua/Shao Rui)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha