Simulizi za Mji | Shannan, "chimbuko la utamaduni wa Xizang": kurithisha utamaduni wa mamia na maelfu ya miaka, kufungua sura mpya ya zama zetu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2026

Shannan inaitwa "Lhoka" katika lugha ya Xizang, ikisifiwa kuwa "mzizi wa kabila la Watibeti, chimbuko la utamaduni wa Xizang." Wastani wa mwinuko wa Eneo hilo juu ya usawa wa bahari unafikia mita 3,700, na mazingira ya asili ya eneo hilo ni kama kazi ya ustadi wa ajabu.

Katika eneo hilo pana, kuna mandhari ya mazingira ya asili, mila na desturi na urithi wa kale, michezo na utamaduni wa umma, pamoja na viwanda vinavyoleta ustawi kwa watu, na vyote hivyo vinaonyesha sura ya Shannan inayochanganya urthi wa jadi na ujenzi wa mambo ya kisasa.

Kila ziwa na mlima vinaunda rasilimali za utamaduni na vivutio vya utalii, kila ufundi na ngoma vinarithisha mila na desturi za maelfu ya miaka, kila mpira na moyo vinaongeza hisia za upendo kati ya watu wa makabila mbalimbali, na kila kiwanda na shughuli vinaimarisha msingi wa kuleta ustawi kwa wakazi. Shannan ya hivi leo inaanzisha mfumo wa maendeleo wa sekta mbalimbali kwa kutegemea rasilimali zake nyingi za utamaduni. Inalinda  mazingira ya uwanda wa juu huku ikitumia vizuri rasilimali zake za urithi wa utamaduni usioshikika na utalii wa kitamaduni.

Shannan inawatolea wakazi huduma za utamaduni na michezo, na kuweka mkazo katika kuendeleza shughuli zake zenye nguvu bora kama vile ufugaji nyuki na utengenezaji wa divai ya uwanda wa juu. Inafanya juhudi kubwa za kuandika ukurasa mpya wa zama zetu kuhusu ustawishaji wa viwanda na maisha ya watu yenye usalama na furaha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha