Lugha Nyingine
Africa CDC yalaani shambulio katikati ya mlipuko wa Ebola nchini DRC
Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC) kimelaani shambulio baya dhidi ya raia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika taarifa yake, Africa CDC imesema shambulio hilo limekuja katika wakati muhimu wa mwitikio wa mlipuko unaoendelea wa Ebola, na hospitali zimeshambuliwa na wagonjwa, wakiwemo mamia ya watu waliothibitishwa ama kushukiwa kuwa na maambukizi ya Ebola, wamekimbia kutafuta usalama, hivyo kuongeza wasiwasi wa afya ya umma.
Taarifa hiyo imesema, shambulio hilo limeripotiwa kufanywa na waasi wa ADF kuanzia Alhamis usiku hadi ijumaa iliyopita katika eneo la Cantine-Aloya, mjini Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini.
Africa CDC imesisitiza haja muhimu ya kuhakikisha ushoroba wa amani, ulinzi wa raia, wagonjwa, wafanyakazi wa afya na vituo vya afya, na pia njia salama na upatikanaji endelevu wa mahitaji kwa jamii zilizoathirika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



