Lugha Nyingine
EAC yazindua mpango wa dharura wa kikanda kukabiliana na El Nino
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imezindua mpango wa kikanda wa dharura kukabiliana na El Nino kwa lengo la kuratibu mwitikio kati ya nchi wanachama wakati ikitabiriwa mvua kubwa kuendelea kunyesha hadi mwezi Februari, 2027.
Taarifa iliyotolewa na makao makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha, Tanzania, imesema mpango huo uliidhinishwa ijumaa iliyopita wakati wa kikao cha ngazi ya mawaziri wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Amani na Usalama na Baraza la Kisekta la Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mpango huo unatoa kipaumbele katika maeneo matano ambayo ni tahadhari ya mapema na hatua za maandalizi, maandalizi na mwitikio wa kiafya, unyumbufu wa miundombinu na utalii, usalama wa chakula, kilimo na maisha, na usafiri na makazi kwa watu wanaoathirika na mabadiliko ya tabianchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



