Lugha Nyingine
Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi wafunguliwa nchini Uturuki

Simon Stiell, katibu mtendaji wa mabadiliko ya tabianchi akihutubia ufunguzi wa COP31 huko Antalya, Uturuki, Novemba 9, 2026. (Mustafa Kaya/Xinhua)
Mkutano wa 31 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) umefunguliwa jana Novemba 9 huko Antalya, Uturuki.
Mkutano huo utafuatilia maeneo matatu muhimu, ikiwa ni pamoja na kutimiza lengo la kupunguza uzalishaji wa hewa chafu, kutoa ufadhili wa sekta ya tabianchi kwa nchi zinazoendelea, na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na hali mbalimbali na ustahimilivu, ili kubadilisha ahadi zilizofanywa katika mikutano iliyopita ya tabianchi kuwa matokeo halisi.
Simon Stiell, katibu mtendaji wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa, alihutubia ufunguzi wa mkutano akisema, asilimia 90 ya miradi mikubwa ya nishati mbadala kwa sasa ni "ya gharama chini zaidi kuliko ile ya nishati za visukuku," akionya kuwa "maendeleo hata hayapo karibu na kuwa haraka au kuwa na haki ya kutosha."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



