China kuendeleza ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja katika Anga za Juu

(CRI Online) Novemba 10, 2026

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun amesisitiza kuwa, China daima inashikilia kutumia anga za juu kwa njia ya amani, kufanya ushirikiano wa kimataifa wa anga za juu, na kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja katika Anga za Juu. Amesema katika historia ya miradi ya usafiri wa anga za juu ya China, itakuwa ni mara ya kwanza kwa mwanaanga wa Pakistan kushiriki katika kazi ya kwenda katika anga za juu, na pia itakuwa mara ya kwanza kwa kituo cha anga za juu cha China kukaribisha mwanaanga wa kigeni.

Guo amesema hayo alipojibu swali katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu taarifa za mwanaanga mmoja wa Pakistan kushiriki katika usafiri wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-24, na baada ya kusafiri kwa muda mfupi atarudi Dunia kwa kutumia chombo cha anga ya juu cha Shenzhou 23.

Guo pia amesisitiza kuwa China iko tayari kuimarisha ushirikiano na Pakistan katika usafiri wa anga za juu na sekta nyingine, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili hadi katika ngazi mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha