Lugha Nyingine
Uganda na Rwanda kufanya zoezi la pamoja la kukabiliana na dharura za afya ya umma
Uganda na Rwanda zitafanya zoezi la pamoja la kuvuka mpaka la mwitikio wa kiafya ili kuimarisha uwezo wao wa kukabiliana na dharura za afya za umma.
Wizara ya afya ya Uganda imetoa taarifa ikisema, zoezi hilo la siku tatu limepangwa kuanza Novemba 11 katika forodha ya Gatuna likiwaleta pamoja maofisa wa afya kutoka nchi mbili na wadau wengine kujaribu uratibu, mabadilishano ya habari na mipango ya rufaa wakati wa dharura za afya ya umma zinazoweza kutokea.
Wizara hiyo imesema, zoezi hilo litatumia hali zinazofanana kutathmini utayari na kuimarisha ushirikiano wa kuvuka mpaka kati ya nchi hizo mbilijirani.
Zoezi hilo litakuwa pamoja na mazoezi yanayohusisha wafanyakazi wa afya na mashirika mengine ya mpakani pamoja na wajumbe wa umma wanaoweza kutazama shughuli hizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



