Mauzo ya kahawa ya Ethiopia yafikia dola za kimarekani milioni 878 katika robo ya kwanza ya mwaka

(CRI Online) Novemba 09, 2026

Jumla ya mapato yaliyotokana na mauzo ya kahawa ya Ethiopia nje ya nchi imefikia dola za kimarekani milioni 878 katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha, ambalo ni ongezeko la asilimia 15 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mamlaka ya Kahawa na Chai ya Ethiopia (ECTA) imesema, ongezeko limetokana na pato la zaidi ya dola za kimarkeni milioni 100 kutoka mauzo ya kahawa hiyo nchini China. Mamlaka hiyo imesema, soko la China limechukua karibu asilimia 12 ya mapato ya jumla ya mauzo ya kahawa ya Ethiopia nje ya nchi, na kuongeza kuwa, tani 15,125 za kahawa ziliuzwa katika soko la China katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu wa fedha wa Ethiopia ulioanza Julai 8.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha