Idadi ya vifo kwenye ajali ya treni Misri yaongezeka hadi 7 huku 112 wakijeruhiwa

(CRI Online) Novemba 09, 2026

Wizara ya Afya na Idadi ya Watu ya Misri imesema idadi ya vifo kutokana ajali ya kugongana kwa treni mbili Jumapili iliyopita katika mkoa wa Giza nchini Misri imeongezeka na kufikia saba, huku wengine 112 wakijeruhiwa.

Wizara hiyo imesema katika taarifa kwamba watu 45 waliruhusiwa kuondoka hospitali baada ya hali zao kuimarika na kupata matibabu ya lazima, huku wengine saba wakitarajiwa kuruhusiwa hivi karibuni. Majeruhi waliobaki walikuwa wakiendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa kitabibu.

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi alisema kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba alikuwa akifuatilia kwa karibu tukio hilo, alitoa rambirambi kwa familia za waathiriwa na kuwatakia majeruhi wapone haraka. Amesema ameelekeza taasisi za serikali kutoa huduma za matibabu, kuchunguza ajali hiyo kwa haraka, na kuwawajibisha watakaobainika kufanya uzembe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha