Sudan Kusini yazindua ofisi ya kwanza ya usajili wa saratani

(CRI Online) Novemba 06, 2026

Sudan Kusini imezindua ofisi ya kwanza ya usajili wa saratani unaotokana na idadi ya watu katika hospitali ya Mafunzo ya Juba, ikiashiria hatua kubwa katika ufuatiliaji wa ugonjwa huo.

Usajili huo utafuatilia aina za saratani, usambaaji na mwelekeo wake ili kutoa mwongozo wa mpango wa huduma za afya unaotokana na ushahidi na mgao wa rasilimali.

Mwakilishi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC) nchini Sudan Kusini Tolbert Geewleh Nyenswah amesema, usajili huo si mfumo wa kurekodi kesi za saratani pekee, bali pia ni msingi wa kutoa maamuzi bora zaidi, huduma bora zaidi za saratani, na hatua zenye ufanisi zaidi katika kulinda afya ya umma.

Kaimu Waziri wa Afya wa nchi hiyo Dak Duop Bichiok amesema, kwa muda mrefu Sudan Kusini imehangaika kupata takwimu za kuaminika za kitaifa kuhusu saratani, hivyo kudhoofisha juhudi za kuelewa mzigo unaotokana na ugonjwa huo na kupanga kwa ufanisi jinsi ya kukabiliana nao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha