Ghana yadai haki baada ya raia wake wawili kuuawa jijini New York, Marekani

(CRI Online) Novemba 06, 2026

Ujumbe wa kidiplomasia wa Ghana jijini New York, Marekani, umedai haki kufuatia vifo vya raia wawili wa Ghana katika jiji hilo ndani ya wiki moja.

Taarifa iliyotolewa na Ujumbe wa Kudumu wa Ghana katika Umoja wa Mataifa jijini New York imeelezea mshtuko na huzuni kufuatia kifo cha kusikitisha cha Joseph Owusu mwenye umri wa miaka 24 katika hali ambayo haijajulikana, ikiwa ni siku chache tu baada ya raia mwingine wa Ghana kuuawa katika jiji hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa ameeleza kushtushwa na kuhuzunishwa na taarifa hizo, na kuzihakikishia familia za wafiwa kuwa serikali ya Ghana itashirikiana na mamlaka husika na serikali ya Marekani kuhakikisha haki inapatikana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha