UM waomba msaada wa dola milioni 8.9 za kimarekani kuwahudumia Waethiopia wanaokimbilia Kenya

(CRI Online) Novemba 06, 2026

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa ombi la msaada wa dola milioni 8.9 za kimarekani ili kukidhi mahitaji ya dharura katika miezi mitatu ijayo kwa makumi ya maelfu ya Waethiopia wanaokimbilia kaskazini mwa Kenya kutokana na mgogoro unaoendelea nchini Ethiopia.

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja huo, Shirika la Uhamiaji la Kimataifa, na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani yamesema, msaada huo unatarajiwa kuwasaidia watu elfu 50, na kwamba yanajiandaa kutoa misaada kwa jumla ya watu elfu 80 wanaotarajiwa kuwasili katika eneo hilo.

Kwenye taarifa nyingine mpya ya kibinadamu iliyotolewa jana jijini Nairobi, Kenya, Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, hali ya usalama ya Moyale iliyoko upande wa Ethiopia bado haijatulia, huku wakimbizi wapya na watafuta hifadhi wanaowasili wakielezea kuongezeka kwa uharibifu wa nyumba za watu na mitaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha