China yaongeza kwa miaka mitano muda wa kutoza ushuru wa kupinga uuzaji wa bei chini na wa kupinga ruzuku kwa NPA kutoka Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2026

Wizara ya Biashara ya China jana Alhamisi ilisema, kuanzia Ijumaa wiki hii, China itarefusha muda kwa miaka mitano wa kutoza ushuru wa kupinga uuzaji wa bei chini na kutoza ushuru wa kupinga ruzuku kwa bidhaa ya propanoli (n-Propanol, NPA) inayoagizwa kutoka Marekani.

NPA ni kemikali ya viwandani inayotumika zaidi kuwa kiyeyushi na dawa muhimu katika uzalishaji wa bidhaa za kemikali.

Kwa mujibu wa nyaraka mbili za uarifu wa wizara hiyo, chini ya hatua ambazo zimepanuliwa, kiasi cha ushuru wa kupinga uuzaji wa bei chini ni kuanzia asilimia 254.4 hadi 267.4, na ushuru wa kupinga ruzuku ni kuanzia asilimia 34.2 hadi 37.7.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kufanya tena ukaguzi juu ya hatua moja ya kupinga uuzaji wa bei ya chini na hatua nyingine ya kupinga ruzuku wakati zikikaribia mwisho wa muda wa utekelezaji. Wizara ya Biashara imesema, kama ikifutwa kwa ushuru huo, vitendo vya uuzaji wa bei ya chini na vya kutoa ruzuku vinavyohusika na uagizaji wa NPA kutoka Marekani vinaweza kuendelea kutokea tena, na huenda itaendelea kudhuru au kuleta hasara kwa viwanda vya nchini China

China ilitoza ushuru huo kwa mara ya kwanza Novemba 2020 kwa muda wa miaka mitano. Kutokana na ombi la wazalishaji wa bidhaa ndani, China ilianzisha ukaguzi juu ya utozaji wa ushuru wa bidhaa wakati wa kukaribia mwisho wa muda wa utekelezaji Novemba 2025.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha