Mwenyekiti wa Bodi ya Qualcomm China: Muunganiko wa AI na sekta za uzalishaji halisi unaleta mabadiliko mapya mjini Shenyang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 06, 2026

Mkutano wa Ubadilishanaji kati ya Vipaji wa Kaskazini-Mashariki mwa Asia (Shenyang) 2026

Mkutano wa Ubadilishanaji kati ya Vipaji wa Kaskazini-Mashariki mwa Asia (Shenyang) 2026

Asubuhi ya tarehe 17 Oktoba, Mkutano wa Ubadilishanaji kati ya Vipaji wa Kaskazini-Mashariki mwa Asia (Shenyang) 2026 pamoja na Mkutano wa AI kuwezesha Viwanda ulifunguliwa katika Jumba la Makumbusho ya Viwanda la China mjini Shenyang.

Katika hafla ya ufunguzi, Meng Pu, Mwenyekiti wa Bodi ya Qualcomm China, alitoa hotuba na kueleza mawazo yake kuhusu jinsi AI inavyoweza kuingia katika viwanda na kubadilika kuwa nguvu halisi za uzalishaji. Kwa maoni yake, Shenyang ni mji wenye msingi imara wa viwanda, na pia unakumbatia kwa bidii teknolojia mpya na sekta mpya, ukiwa umejenga msingi mzuri wa sekta katika nyanja za roboti na utengenezaji wa ksiasa, na wakati huo huo unaweka mikakati katika nyanja zinazochipuka kama AI kwenye roboti (embodied AI). Mwaka huu mkutano umechukua uwezeshaji wa maendeleo kwa AI kama mada muhimu, na Meng Pu anahisi kuwa “inapatana kabisa na mwelekeo wa maendeleo ya sekta kwa sasa”.

Hivi sasa, AI inaharakisha kuelekea matumizi ya viwandani kutoka uvumbuzi wa teknolojia, na Shenyang nayo inahimiza mabadiliko ya kisasa na ya kidijitali ya sekta ya utengenezaji. Meng Pu alisema kuwa kwa upande mmoja, uwezo wa utengenezaji wa hali ya juu unaendelea kupanda; kwa upande mwingine, teknolojia mpya kama AI, magari ya kisasa na roboti zinaendelea kwa kasi. Pale uvumbuzi wa teknolojia, msingi wa viwanda, matumizi na bidhaa vinapounganishwa kwa karibu zaidi, AI inaweza kuelekea haraka zaidi kutoka teknolojia hadi bidhaa, na kutoka bidhaa hadi uzalishaji na maisha halisi. Na mazingira kama hayo ya uvumbuzi yanazidi kujitokeza zaidi mjini Shenyang na Mkoa wa Liaoning.

Meng Pu, Mwenyekiti wa Bodi ya Qualcomm China

Meng Pu, Mwenyekiti wa Bodi ya Qualcomm China

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha