Libya yapokea hati ya utambulisho ya WHO kwa kutokuwa na ugonjwa wa polio

(CRI Online) Novemba 05, 2026

Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Libya kimesema, nchi hiyo imepokea hati rasmi ya utambulisho kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kutokana na juhudi zake endelevu za kudumisha kutokuwa na ugonjwa wa polio.

Utambulisho huo uliwasilishwa katika barua rasmi iliyoandikwa jumamosi iliyopita kutoka Tume ya Kikanda ya Hati ya Kutokomeza Polio iliyo chini ya Ofisi ya Kanda ya Mediterranean Mashariki kwa Kamati ya Kitaifa ya Hati ya Libya.

Kituo hicho kimesema, utambuzi huo unaakisi ahadi ya Libyaya vigezo vya usimamizi wa magonjwa na mradi wa ufanisi wa kitaifa wa chanjo, pamoja na juhudi zinazoendelea kulinda afya ya umma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha