Lugha Nyingine
Benki ya Dunia yapandisha makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Kenya kwa mwaka 2026
Ripoti ya 34 ya Mtazamo wa Uchumi wa Kenya iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema kuwa kulingana na kasi yake ya 2025, ukuaji wa pato la ndani la Kenya (GDP) unatarajiwa kuwa thabiti kwa asilimia 4.6 mwaka 2026.
Ripoti hiyo iliyotolewa jana jijini Nairobi, imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, ukuaji halisi wa Pato la Ndani la Kenya uliongezeka hadi asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.9 ya mwaka jana kipindi kama hicho, ambapo ukuaji thabiti wa sekta za viwanda na huduma umechangia zaidi ukuaji wa uchumi licha ya kasi ndogo ya ukuaji kwenye sekta ya kilimo.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa ukuaji wa viwanda wa Kenya uliongezeka hadi asilimia 4.9 katika nusu ya kwanza ya 2026, ukichochewa na sekta za ujenzi na utengenezaji, huku sekta ya huduma ikidumisha upanuzi thabiti wa asilimia 5.2, kutokana na utalii, huduma za kifedha, na elimu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



