Mauzo ya Zimbabwe nje yaongezeka kwa asilimia 61 katika robo tatu za kwanza za 2026

(CRI Online) Novemba 05, 2026

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini Zimbabwe (ZimTrade) imesema, thamani ya mauzo ya bidhaa za Zimbabwe nje ya nchi imeongezeka kwa asilimia 61 katika robo tatu za kwanza za mwaka 2026 na kufikia dola bilioni 10.4 za kimarekani.

Akizungumza jana katika Semina ya Wiki ya Wauzaji na Wanunuzi iliyofanyika Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, ofisa mkuu mtendaji wa ZimTrade Allan Majuru amesema mauzo ya bidhaa zilizoongezwa thamani yameongezeka kwa asilimia 68 na kufikia dola milioni 671 za kimarekani, kiasi kinachozidi dola milioni 400 za kimarekani mwaka jana wakati kama huo.

Majuru pia amesisitiza umuhimu wa kupanua uchakataji wa ndani wa maliasili, ili kuhimiza mchango unaotolewa na viwanda vya ndani kwa ukuaji wa uchumi na utoaji wa ajira.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha