Lugha Nyingine
Tanzania kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme hadi megawati 15,000 ifikapo 2031
Tanzania inalenga kuongeza uwezo wa uzalishaji wake wa umeme hadi kufikia megawati 15,000 ifikapo mwaka 2031, kutoka megawati 4,646 za sasa, wakati nchi hiyo ikitafuta kuimarisha usalama wa nishati na kuongeza kasi ya maendeleo ya viwanda.
Waziri wa Nishati nchini humo Juma Homera ametangaza lengo hilo wakati wa kikao cha ngazi ya mawaziri katika Maonyesho na Mkutano wa Kimataifa wa Mafuta unaofanyika Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nishati ya Tanzania jumanne wiki hii, Homera amesema kuongezeka kwa uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini humo kunatokana na kukamilika kwa Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, ambao umewezesha kuongeza uwezo uliopo na kufikia megawati 4,646.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



