China Yapanua Upatikanaji wa Habari na kuwanufaisha Watu wenye ulemavu na Wazee

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2026

Tarehe 26 Oktoba 2025, katika mkahawa wa Trojan Fairy wa Beijing, watu kadhaa wenye ulemavu walizungumza baada ya onyesho la filamu kumalizika. (Xinhua/Yin Gang)

Tarehe 26 Oktoba 2025, katika mkahawa wa Trojan Fairy wa Beijing, watu kadhaa wenye ulemavu walizungumza baada ya onyesho la filamu kumalizika. (Xinhua/Yin Gang)

Habari zimeripoti kuwa China inapanua upatikanaji wa habari, hasa katika maeneo yanayohusiana kwa karibu na maisha ya kila siku ya watu wenye ulemavu na wazee.

Jana Jumanne, ripoti ya utekelezaji wa Sheria ya Ujenzi wa Mazingira Yasiyo na Vizuizi ya China iliwasilishwa kwa kuthibitishwa na Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China, ambalo ni chombo cha juu cha utungaji wa sheria cha China.

Ripoti hiyo inasema kuwa upatikanaji wa huduma za habari na mawasiliano ya habari unatarajiwa kuongezeka katika ubora wao na maeneo zinakofikika.

Ilipofika mwisho wa mwaka 2025, tovuti 11,000 hivi zinazoendeshwa na ofisi za chama na idara za serikali zilikuwa zimeboreshwa ili kuongeza upatikanaji, na zaidi ya tovuti na programu za simu 3,100 zinazotumiwa mara kwa mara na watu wenye ulemavu na wazee zilifanyiwa maboresho ili kuwahudumia vizuri zaidi.

Ripoti hiyo inasema kuwa matumizi ya teknolojia ya AI katika huduma za upashanaji wa habari zisizo na vizuizi pia yanazidi kupanua, na AI inatumika katika matangazo ya lugha ya ishara na miundombinu isiyo na vizuizi.

Sheria ya Ujenzi wa Mazingira Yasiyo na Vizuizi ilianza kufanya kazi Septemba 2023, na ni sheria ya kwanza ya China inayolenga mahsusi ujenzi wa mazingira yasiyo na vizuizi, ikiweka kanuni kwa mfumo kamili kuhusu miundombinu isiyo na vizuizi, upashanaji wa habari na mawasiliano ya habari, na huduma za umma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha