Lugha Nyingine
Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la 2026 la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” Lafanyika Fuzhou, China

Picha inaonyesha eneo la hafla ya ufunguzi ya Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la 2026 la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" huko Fuzhou, kusini-mashariki mwa Mkoa wa Fujian, China. (Picha na Zhang Wujun)
Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la 2026 la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilifanyika tarehe 3 Novemba huko Fuzhou, kusini-mashariki mwa Mkoa wa Fujian, China.
Tukio hilo lilileta pamoja zaidi ya wawakilishi 200 wa kigeni kutoka nchi 100, pamoja na mashirika ya kimataifa na ya kikanda, na vyombo na taasisi 182 za habari.
Washiriki walibainisha kuwa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kutoka pendekezo la China hadi vitendo vya kimataifa, umekuwa bidhaa ya umma ya kimataifa inayokubalika na jukwaa kubwa zaidi la kimataifa la ushirikiano wa kiuchumi kwa ukubwa wake, wigo wake na athari yake.
Washiriki wanaamini kuwa vyombo vya habari kutoka nchi mbalimbali vinapaswa kushirikiana ili kurekodi na kushiriki simulizi za kuvutia za Njia ya Hariri, kuwezesha mawasiliano ya kisera na mabadilishano baina ya watu, na kukuza mazingira mazuri ya maoni ya umma.

Picha inaonyesha hafla ya ufunguzi ya Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari la 2026 la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” huko Fuzhou, kusini-mashariki mwa Mkoa wa Fujian, China. (Picha na Zhang Wujun)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



