Kenya kutumia maonyesho ya CIIE kuongeza mauzo yake China

(CRI Online) Novemba 03, 2026

(Picha/Xinhua)

Ofisa mkuu mtendaji wa Shirika la Utangazaji wa Bidhaa na Chapa za Kenya Kwa Nje, Bi. Floice Mukabana. (Picha/Xinhua)

Ofisa mkuu mtendaji wa Shirika la Utangazaji wa Bidhaa na Chapa za Kenya Kwa Nje, Bi. Floice Mukabana, amesema Kenya itatumia ushiriki wake katika Maonyesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yatakayofanyika Shanghai, kuongeza mauzo ya nje ya bidhaa kuu za kilimo kwenye soko la China.

Bi. Mukabana amesema maonyesho CIIE yanatoa jukwaa la kimkakati kwa makampuni mapya ya Kenya kuonyesha bidhaa zenye thamani kubwa, zinazoweza kufuatiliwa na kuthibitishwa katika soko kubwa la China, huku ikijenga uhusiano wa muda mrefu na wanunuzi, waagizaji na wasambazaji.

Amesema maonyesho hayo yanawaleta pamoja waagizaji, wasambazaji, waendeshaji wa biashara ya mtandaoni na wasimamizi wa China, na kuwezesha makampuni ya Kenya ya ukubwa wote kupata maarifa kuhusu vigezo vinavyohitajika vya kuingia soko la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha