Mkutano wa 38 wa Wanachama wa Itifaki ya Montreal wafunguliwa Rwanda

(CRI Online) Novemba 03, 2026

Mkutano wa 38 wa Wanachama wa Itifaki ya Montreal umefunguliwa Jumatatu huko Kigali nchini Rwanda.

Mkutano huo utakaofanyika hadi Ijumaa unawashirikisha wajumbe kutoka serikali, mashirika ya kimataifa, sekta ya viwanda na washirika wengine, kwa lengo la kuendeleza juhudi za dunia katika kuhifadhi Tabaka la Ozoni, na kuimarisha ushirikiano juu ya mabadiliko ya tabianchi.

Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mazingira wa Rwanda Bernadette Arakwiye amesema, mkutano huo unaadhimisha Marekebisho ya Kigali yaliyopitishwa miaka kumi iliyopita, ambayo yanaahidi kuwa nchi mbalimbali zitapunguza matumizi ya gesi ya hydrofluorocarbons (HFCs) hatua kwa hatua.

Ametoa wito kwa nchi mbalimbali kuunga mkono Azimio la Kigali+10, linalotaka nchi zitumie mbinu endelevu za kupoza, na kuhakikisha pande zote zina fedha, teknolojia, uwezo na taasisi vinavyohitajika katika utekelezaji wa Marekebisho ya Kigali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha