Standard Bank kuongoza ujumbe wa wafanyabiashara wa Afrika kwenye Maonyesho ya 9 ya CIIE

(CRI Online) Novemba 03, 2026

Kundi la Standard Bank lilitangaza Jumatatu kuwa litaongoza ujumbe wa wafanyabiashara 20 kutoka nchi saba za Afrika kwenye Maonyesho ya 9 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), kwa lengo la kuwaunganisha wauzaji bidhaa wa Afrika na wanunuzi, wawekezaji, na washirika wa kibiashara wa China.

Taarifa iliyotolewa na benki hiyo inasema ujumbe huo unajumuisha biashara kutoka Afrika Kusini, Ghana, Nigeria, Kenya, Malawi, Tanzania, na Uganda, biashara ambazo kwa kiasi kikubwa zinajihusisha na sekta ya kilimo na uchakataji wa mazao ya kilimo, zitaonyesha bidhaa mbalimbali ikiwemo kahawa, kakao, chai, mvinyo, parachichi, korosho, ufuta, na nafaka.

Ofisa mwandamizi wa benki hiyo Bw. Luthando Vuba amesema maonyesho hayo yanayofanyika kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 10, ni jukwaa muhimu kwa wafanyabiashara wa Afrika kuwasiliana moja kwa moja na wanunuzi, wasambazaji, wawekezaji, na washirika wa kimkakati wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha