Lugha Nyingine
Xi afanya mazungumzo na Sultani wa Oman, akisisitiza ushirikiano wa pande mbili na juhudi za amani katika Mashariki ya Kati

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Sultani Haitham Bin Tarik Al Said wa Oman, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 2 Novemba 2026. (Xinhua/Li Xiang)
BEIJING - Rais Xi Jinping amesema kuwa China inapenda kufanya juhudi za pamoja na Oman, kuinua uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwenye kiwango cha juu zaidi, na kusaidia kurejesha mapema iwezekanavyo amani ya Mashariki ya Kati na kutimiza utulivu wa kudumu.
Xi ameyasema hayo jana Jumatatu kwenye mazungumzo na Sultani Haitham Bin Tarik Al Said wa Oman, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China. Hii ni mara ya kwanza kwa mkuu wa nchi ya Oman kufanya ziara nchini China tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili katika miaka 48 iliyopita.
"Mazungumzo haya ni ukurasa muhimu katika historia ya uhusiano kati ya China na Oman, na yataingiza msukumo mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano wa pande mbili," amesema Xi.
Amesema China na Oman zinapaswa kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa na kuimarisha kubadilishana uzoefu katika utawala wa nchi, wakati huohuo ameeleza uungaji mkono wa China kwa Oman katika kulinda uhuru, mamlaka ya nchi, usalama na utulivu, na kutafuta kwa kujiamulia njia ya maendeleo inayolingana na hali halisi ya nchi yake.
"Pande mbili zinapaswa kupanua ushirikiano wa kivitendo na kuimarisha siku hadi siku msingi wa ushirikiano wa kunufaishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja," amesema, akiongeza kuwa China imefanya juhudi zaidi za kuhimiza maendeleo yenye sifa bora na kupanua ufunguaji mlango kwa vigezo vya juu, na juhudi hizo zitatoa fursa kubwa zaidi kwa Oman na nchi nyingine.
Xi amesema China inalenga kuufanya ushirikiano wa pande mbili katika sekta ya nishati kuwa wa mambo mbambali na kwa pande zote, kuimarisha ushirikiano katika viwanda, uwekezaji, AI, sayansi na teknolojia, pamoja na mawasiliano kati ya watu, na pia kushirikiana katika njia ya kuelekea maendeleo, ustawishaji, na ujenzi wa mambo ya kisasa.
Xi ameeleza kuwa Mashariki ya Kati na eneo la Ghuba havipaswi kuwa uwanja wa ushindani kati ya nchi kubwa au migogoro ya siasa za kijiografia, na kilicho muhimu ni kufanya juhudi za pamoja za kuhimiza na kudumisha amani na utulivu kwenye eneo hilo.
"China itaendelea kutetea utatuzi wa migogoro wa kupitia njia za kisiasa na kidiplomasia, na inaunga mkono nchi za kikanda katika kujenga maskani ya pamoja yaliyo ya ujirani mwema, urafiki, maendeleo ya pamoja, usalama na ushirikiano," ameongeza.
Kwa upande wake Sultan Haitham Bin Tarik amesema kuwa Oman inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaiunga mkono China katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi.
Ameelezea matumaini yake kuwa ziara yake hiyo itakuwa mwanzo mpya katika kutafuta fursa zaidi za ushirikiano na China, kujenga uhusiano wa washirika wa kuelekea siku za baadaye, na kusukuma mbele maendeleo makubwa zaidi ya uhusiano wa pande mbili.
Amesema kuwa Oman inasifu sana msimamo wa haki wa China juu ya suala la Mashariki ya Kati, na inapenda kudumisha uratibu wa karibu na China, kushikilia kwa pamoja sheria za kimataifa, kutetea kutatua migogoro kwa njia ya amani, na kwa pamoja kuhimiza usalama na utulivu kwenye eneo hilo na kwingineko.

Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Sultani Haitham Bin Tarik Al Said wa Oman, ambaye anafanya ziara ya kiserikali nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, tarehe 2 Novemba 2026. (Xinhua/Ding Lin)

Baada ya kufanya mazungumzo yao mjini Beijing, Rais wa China Xi Jinping na Sultani Haitham Bin Tarik Al Said wa Oman kwa pamoja wakishuhudia utiaji saini wa nyaraka za ushirikiano katika sekta ya viwanda, minyororo ya utoaji wa bidhaa, maendeleo ya kijani, na mambo ya fedha ya kidigitali, tarehe 2 Novemba 2026. (Xinhua/Gao Jie)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Sultani Haitham Bin Tarik Al Said wa Oman kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, tarehe 2 Novemba 2026. (Xinhua/Yue Yuewei)

Rais wa China Xi Jinping akifanya hafla ya kumkaribisha Sultani Haitham Bin Tarik Al Said wa Oman kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, tarehe 2 Novemba 2026. (Xinhua/Gao Jie)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



