China yatoa mafunzo ya AI kwa wataalamu wa vyombo vya habari wa Tanzania

(CRI Online) Novemba 02, 2026

Mamlaka ya Kitaifa ya Redio na Televisheni ya China (NRTA) Jumapili yalifanya programu ya mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa vyombo vya habari wa Tanzania, ili kuongeza uwezo wao wa kidigitali, kuboresha uzalishaji wa maudhui, na kutafuta fursa mpya za kibiashara.

Programu hiyo iitwayo “mafunzo ya AI kwa vyombo vya habari kati ya China na Afrika” ilifanyika Dar es Salaam, ikiwashirikisha wataalamu takriban 30 wa sekta ya habari.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema AI inabadili kwa kasi sekta ya habari. China imedhamiria kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza uwezo wa kidigitali na kupunguza pengo la kidigitali, akisisitiza kuwa maendeleo ya AI yanapaswa kuwa shirikishi na kuwanufaisha watu wote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha