Mpango wa China wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia ya Ghuba ya Bluu wasifiwa na UN kuwa mradi mkubwa muhimu wenye uwakilishi duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2026

Mpango wa China wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia ya Ghuba ya Bluu ukisifiwa na Umoja wa Mataifa kuwa Mradi Mkubwa Muhimu Wenye Uwakilishi wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia Duniani, kwenye mkutano wa 17 wa Nchi Wasaini wa Mkataba wa Anuwai ya Viumbe (COP17) uliofanyika Yerevan, Armenia, tarehe 29 Oktoba, 2026. (Xinhua/Chen Junfeng)

Mpango wa China wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia ya Ghuba ya Bluu ukisifiwa na Umoja wa Mataifa kuwa Mradi Mkubwa Muhimu Wenye Uwakilishi wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia Duniani, kwenye mkutano wa 17 wa Nchi Wasaini wa Mkataba wa Anuwai ya Viumbe (COP17) uliofanyika Yerevan, Armenia, tarehe 29 Oktoba, 2026. (Xinhua/Chen Junfeng)

YEREVAN - Mpango wa China wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia ya Ghuba ya Bluu umesifiwa na Umoja wa Mataifa kuwa Mradi Muhimu Mkubwa Wenye Uwakilishi wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia Duniani, jana Alhamisi, kwenye mkutano wa 17 wa Nchi Wasaini wa Mkataba wa Anuwai ya Viumbe (COP17) uliofanyika Yerevan, Armenia.

Mpango huo umeandaliwa kwa uhimizaji wa pamoja wa Wizara ya Maliasili na Wizara ya Fedha ya China. Hii ni mara ya pili kwa mpango wa China wa urejeshaji wa hali ya ikolojia kote nchini kupata utambuzi wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Urejeshaji wa Miaka 10 wa Mifumo ya Ikolojia, na kuifanya China kuwa nchi ya kwanza kupata heshima hiyo mara mbili.

Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), amesema kuwa Mpango huo wa Urejeshaji wa Hali ya Ikolojia ya Ghuba ya Bluu uliochaguliwa kutoka kwenye maombi zaidi ya 200 na uteuzi wa kiserikali zaidi ya 80 na umetambuliwa kuwa moja ya mifano bora duniani yenye matumaini zaidi, ni mpango kabambe zaidi yenye azma na ari kubwa zaidi inayotoa hamasa zaidi katika urejeshaji wa mifumo ya ikolojia.

Ameongeza kuwa mpango huo unalenga kurejesha ardhi oevu kwa hekta zaidi ya 150,000 kwenye maeneo ya pwani, na kilomita zaidi ya 2,000 za sehemu za mwambao wa bahari ifikapo mwaka 2030 kwa ajili ya kuleta manufaa ya kudumu kwa maeneo ya wakazi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Renato Lu)

Picha