Lugha Nyingine
Mkutano wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya CPC wamalizika, ukipitisha azimio la kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote

Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC mjini Beijing. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano wake wa tano wa wajumbe wote, ulioongozwa na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi wiki hii mjini Beijing, ambapo imepitisha azimio la kushikilia kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo imeeleza kuwa Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, alitoa hotuba muhimu.
Kwenye mkutano huo, washiriki walisikiliza na kujadili ripoti aliyotoa Xi juu ya kazi za Ofisi ya Siasa.
Pia walijadili na kupitisha Azimio la Kamati Kuu ya CPC la Masuala Makubwa Kuhusu Kujiendesha Chama kwa Nidhamu kali Kwa Pande Zote. Xi alitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya mswada wa azimio hilo. Taarifa hiyo imesema kuwa Kamati Kuu ya CPC imethibitisha vya kutosha kazi iliyofanywa na Ofisi ya Siasa tangu mkutano wa nne wa wajumbe wote wa kamati kuu hiyo.
Kwa kukumbuka historia na safari ya Chama tangu kuanzishwa kwake, Kamati Kuu ya CPC imeeleza kuwa umuhimu kwa Chama cha CPC kujipatia ushindi mmoja baada ya mwingine ulitokana na matumaini makubwa ya chama hicho ya kufuata wazo la ukomunisti, kufanya juhudi zaidi za kutimiza lengo la kujenga ukuu wa kudumu kwa taifa la China, na kushikilia kutafuta ustawi kwa watu wa China na kutafuta ustawishaji wa taifa la China.
Kwenye mkutano huo, Kamati Kuu ya CPC ilisifu zaidi mafanikio makubwa kiliyoyapata Chama katika kujiendesha kwa nidhamu kali kwa pande zote katika zama mpya. Ilielezwa kuwa, wakati Chama kikijitahidi kujisimamia, kujiendesha, kujiendeleza, na kujiimarisha katika zama mpya, Kamati Kuu ya CPC, ikiongozwa na Komredi Xi Jinping, imetoa mfululizo wa mawazo mapya, fikra mpya, na mikakati mipya juu ya masuala makubwa ya zama za hivi sasa kuhusu Chama cha CPC kinapaswa kujijenga kuwa chama tawala cha muda mrefu cha Umarx cha namna gani, na kukijenga kwa mbinu za namna gani, ndiyo maana imetolewa kwa fikra ya Xi Jinping kuhusu ujenzi wa Chama.
Taarifa ya mkutano huo "Ilisisitiza kuwa hivi sasa yapo mazingira mengi mazuri yanayoweza kusaidia kusukuma mbele Chama kujisimamia kwa nidhamu kali kwa pande zote, wakati huohuo pia tunakabiliwa na hali nyingi mpya pamoja na matatizo mapya katika jitihada hii".
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mabadiliko makubwa yametokea katika dunia nzima, nchini China na katika hali ya Chama, mabadiliko hayo yameleta hali ngumu zaidi kwa majukumu ya Chama cha CPC ya kushikamana na wananchi na kuwaongoza katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama, na maslahi ya maendeleo ya China; kushikamana na wananchi na kuwaongoza katika kuhimiza mageuzi na maendeleo na kudumisha hali ya masikilizano na utulivu kwenye jamii; pamoja na kudumisha sifa ya utangulizi na kufuata maadili bila ufisadi.

Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ukiongozwa na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ukifanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Yue Yuewei)

Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi wakihudhuria kwenye Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofanyika mjini Beijing. (Xinhua/Li Xiang)

Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi wakihudhuria Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofanyika mjini Beijing. (Xinhua/Li Xiang)

Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ulioongozwa na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC ukifanyika mjini Beijing. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Mkutano wa tano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ukifanyika mjini Beijing. (Xinhua/Zhai Jianlan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



