Rais wa China atoa rambirambi kuhusu ajali ya treni iliyosababisha vifo nchini Hispania

(CRI Online) Oktoba 30, 2026

Rais Xi Jinping wa China Alhamisi wiki hii alituma ujumbe wa rambirambi kwa Mfalme wa Hispania Felipe VI kufuatia vifo vilivyotokea kwenye ajali ya kugongana kwa treni za mwendo kasi iliyotokea katika mkoa wa Toledo nchini Hispania.

Katika ujumbe huo, Rais Xi ametoa salamu za rambirambi za dhati kwa familia zilizopoteza wapendwa wao kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, baada ya kufahamu kuwa ajali hiyo imesababisha vifo na majeruhi wengi. Pia amewatakia majeruhi wa ajali hiyo wapone haraka.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha