Lugha Nyingine
Kuona Siku za Baadaye Shenzhen, China | Siku Moja ya Mikono Miwili ya Roboti ya Kuchanganua Vifurushi
Hii ni ratiba ya kila siku ya mikono miwili midogo ya roboti kwenye mstari wa kupitisha vifurushi vya kupelekwa kwa wateja: inageuza lebo za taarifa za usafirishaji, kunyoosha vifurushi, na hata kuondoa "vifurushi visivyohitajika." Iachie kazi za kuchosha na zinazojirudia-rudia—ili binadamu waweze kujikita kwenye mambo ya uvumbuzi zaidi!
Mikono hii miwili ya roboti "yenye bidii" inatoka kampuni ya Teknolojia ya Roboti ya Shenzhen Zibianliang. Mkutano wa 33 wa Viongozi wa Uchumi wa APEC umepangwa kufanyika mjini Shenzhen, China, kuanzia tarehe 18 hadi 19 Novemba. Hivi karibuni, kundi la waandishi wa habari kutoka China na mataifa mengine—wakiwa sehemu ya mpango wa "Kuikaribisha APEC: Waandishi wa Habari Kutembelea Shenzhen"—walitembelea mji huo ili kujionea kwa karibu hali moto moto ya uvumbuzi wa kiteknolojia katika mambo ya biashara. Imeonekana dhahiri kwamba, taswira ya siku za baadaye inaweza kupatikana hapa hapa, kwenye mikono hii ya roboti isiyochoka kamwe. (Yang Qian)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



