Lugha Nyingine
Xi ampongeza Lula kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Brazil
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amempongeza Luiz Inacio Lula da Silva kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Brazil.
Katika pongezi lake lililotolewa jana Jumanne, Xi amesema kuwa Rais Lula ametoa mchango muhimu katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Brazil.
Xi amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, yeye na Lula wamedumisha mawasiliano ya karibu kupitia njia mbalimbali na kwa pamoja wameongoza ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja kwa ajili ya maendeleo mapya yanayopatikana katika dunia ya haki zaidi na sayari ya dunia ya endelevu zaidi.
Amesema uhusiano wa pande mbili ulio wa kidunia, kimkakati na wa muda mrefu umeonesha umuhimu wake zaidi, hali ambayo imeufanya uwe mfano wa mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za Kusini mwa Dunia.
Xi amesema ametilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Brazil na anapenda kushirikiana na Rais Lula katika kuhimiza pamoja ujenzi wa jumuiya ya China na Brazil yenye mustakabali wa pamoja kufikia kiwango kipya, kufungua matarajio mapana zaidi kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya nchi hizo mbili, na kuendelea kuboresha siku hadi siku ustawi wa watu wa nchi zote mbili.
Siku hiyo ya Jumanne, Makamu Rais wa China Han Zheng, pia alituma salama za kumpongeza Geral do Alckmin kuchaguliwa tena kuwa rais wa Brazil.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



